Kanisa la Waadventista Wasabato Moria lilipangwa kuwa kanisa kutokea kanisa la Swebo mtaa wa Kiwira tarehe 30/08/2013 likiwa na jumla ya waumini 98. Kanisa hili lipo kwenye kijiji cha Ntokela kata ya Isongole na wilayani Rungwe, kando kando ya barabara ya lami itokayo Uyole Mbeya ielekeayo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Malawi. Umali wake kutokea Uyole ni maili 30 na umbali wake kutokea mji mdogo wa Kiwira ni Maili kumi hivi. Unapokuja kututembelea utashukia kwenye kituo maarufu kijulikanacho kama Msasani. Kanisa hili lilianza kama kundi likijulikana kama kundi la Msasani jina lililodumu kwa miezi kadhaa hadi tulipopewa hadhi ya kuwa Kanisa na kuchagua kuliita kanisa letu Moria. Jina la Moria linatokana na kumbukumbu ya mlima ambao Ibrahimu yule baba wa Imani alipotoa kafara ya mwanawe Isaka - kafara iliyosimama badala ya Kafara ya Mwana wa Mungu - yaani Yesu Kristo. Viongozi Waasisi wa kanisa hili ni 1. Benjamini Sanga 2. Hadsoni Solomoni, na 3. Dackson Sanga.![]()